September 27, 2015


Nahodha wa Mbeya City, Juma Nyosso amerudia yaleyale baada ya kumdhalilisha nahodha wa Azam FC, John Bocco.


Nyosso amempisha makalio Bocco wakati wa mechi ya Ligi Kuu Bara ambayo Azam FC ilishinda mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.

Nyosso aliwahi kumfanyia hivyo mshambuliaji Elius Maguri wakati akiwa Simba, lakini akaomba radhi.


Lakini leo amerudia kwa makusudi kumfanyia hivyo Bocco hali iliyozua tafrani kubwa mwamuzi Martin Saanya naye akashiriki kuamua lakini akataka kujua ukweli wa jambo hilo baada ya malalamiko ya Bocco kutokana na kitendo hicho kibaya cha Nyosso ambaye ameonekana kamwe si mtu wa kubadilika.


Bocco alionekana kuchukizwa na tukio hilo la Nyosso na kutaka kumvaa lakini wachezaji wa Azam FC akiwemo Kipre Tchetche walifanya kazi ya ziada kuwatenganisha.

Hata hivyo, Nyosso alionekana kuwa mkorofi akipinga kwamba hajafanya hivyo.

Baada ya kuona mambo ni magumu, Nyosso ambaye ni nahodha alianza kumbembeleza Bocco ambaye kamwe hakukubaliana na jambo hilo.

Mara ya kwanza, Blog hii ilimuanika Nyosso akimfantia Maguri kitendo kama hicho, akaomba radhi lakini TFF ikamfungia mechi nane.


Lakini yeye akaendeleza kusema anajutia jambo hilo kabla ya leo kurejea kufanya upuuzi huo kwa mara nyingine.

Benchi la ufundi la Azam FC walipeleka ushahidi wa Nyosso kufanya hivyo kwa mwamuzi wa akiba na baadaye kamisaa na sasa suala hilo litafika tena TFF.

Mara ya kwanza, bolog hii na gazeti la CHAMPIONI lilipoanika uozo wa Nyosso wengi walipinga. Lakini leo imedhirika kwamba ni mtu anayestahili adhabu kali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic