![]() |
| MGOYI (WA PILI KUSHOTO) AKIZUNGUMZA JAMBO HUKU AKISIKILIZWA NA RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI NA WADAU WENGINE. |
Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kimezindua rasmi kozi ya
ukocha wa leseni C’ inayotambuliwa na Caf.
Kozi hiyo ya wiki mbili iliyozinduliwa jana inaendeshwa na
mkufunzi, Salum Madadi ambaye ni Mkurugenzi wa ufundi wa TFF, ikiwa na jumla ya
washiriki 31 wengi wao wakiwemo makocha wa vilabu vya ligi daraja la
pili,daraja la kwanza na ligi kuu.
Miongoni mwa washiriki hao ni pamoja na
kocha msaidizi wa Simba, Suleiman Matola, katibu mkuu wa zamani wa Simba Muhina
Kaduguda, Kocha wa Ruvu shooting Tom Olaba, Kocha wa makipa wa Yanga, Juma
Pondamali, nyota wa zamani wa Taifa Stars, Ally Mayai na Peter Tino.
| MWENYEKITI WA DRFA, KASONGO ALMASI AKIZUNGUMZA JAMBO. |
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa kozi hiyo
ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Tff, Msafiri Mgoyi,ambaye amewapongeza
washiriki kwa uamuzi wao wa kutaka kujiongezea maarifa ya ufundishaji wa soka
,kwa kuwa tanzania inakabiliwa na upungufu mkubwa wa makocha ikilinganishwa na
mataifa mengine ya Afrika ambayo yamepiga hatua kisoka.
Aidha amesema Tff imeweka mpango maalum wa
kutunza kumbukumbu za makocha hao na wengine watakaopatikana,pamoja na
kufuatilia kazi zao kwenye vilabu mbalimbali watakavyofundisha ili iwe rahisi
kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufanya kazi zao.
Naye, Mwenyekiti wa DRFA, Almasi Kasongo
wakati akimkaribisha mgeni rasmi,amesema chama chake kinataraji pia kuendesha
kozi za madaktari pamoja na kuendeleza mpango wake wa kuinua soka la vijana,ili
taifa liwe na wachezaji wenye uwezo wa kushindana na mataifa mengine.
Kasongo amesema licha ya chama chake kuwa
na mikakati ya kuhakikisha soka la mkoa wa Dar es salaam na nchi kwa ujumla
linanyanyuka,lakini bado nguvu kumbwa inahitajika kutoka Tff pamoja na wadau
wenye mapenzi mema na mpira wa nchi hii.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI NA
MAWASILIANO YA DRFA,
Omary Katanga,
Mkuu wa habari na mawasiliano DRFA.








0 COMMENTS:
Post a Comment