September 10, 2015


Baada ya mkataba wa Sh bilioni 3.3 wa Azam Media Group kwa TFF kuidhamini michuano ya Kombe la FA Tanzania, Ofisa Mtendaji, Rhys Torrington alitoa maelezo yake.


Soma hapa upate alichokielezea:

 “Huu ni wakati muhimu kwa wapenzi wa kandanda hapa Tanzania na pia ni mapinduzi ya matangazo luninga. 

Nimekuwa nikisema mara zote kuwa lengo letu ni kuufanya mchezo huu kuwa sehemu nzuri ya burudani kuliko shindano linalomalizika ndani ya muda mfupi.”  

Alipoulizwa kuhusu jina la michuano hiyo  amesema: 

“Limekuwa jambo zuri kuwa michuano hii mipya itabeba jina la chaneli yetu ya Azam Sports ambayo inatoa fursa kwa watazamaji kuona pia michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom, La Liga na sasa michezo ya ASFC moja kwa moja katika picha ang’avu zaidi. 

"Pamoja na makubaliano ya karibuni  ya kuwa mshirika rasmi wa TFF kwa matangazo ya michezo ya kimataifa ambayo wana haki, hatua hii inaimarisha uhusiano wa pande mbili hizi kwa manufaa ya michezo hapa Tanzania”.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi ameeleza matumaini yake juu ya shindano hilo jipya: “Kwa muda mrefu nimekuwa nikihitaji Tanzania kuwa na aina yake ya Kome la FA na sasa, kwa kuungwa mkono na  Azam Media, siku hii imewadia .

"Uzoefu wa kufanya kazi nao kwa zaidi ya miaka miwili sasa na kufanya VPL  kuonekana kwa mashabiki nchini kote umedhihirisha kuwa ni washirika muhimu,na wana dhamira kama ya TFF ya kuboresha kandanda la Tanzanian kadiri iwezekanavyo”.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic