Azam Media Limited
imeingia mkataba wa miaka minne na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kudhamini
michuano ya Kombe la Shirikisho.
Michuano hiyo ambayo
ilijulikana kama Kombe la Fat au FA
itadhaminiwa na kampuni hiyo kuwa ya mambo ya habari kwa thamani ya Sh bilioni
3.3.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi ameshindwa kuficha furaha yake kutokana na udhamini huo mnono wa Azam Media.
KOCHA WA FRIENDS RANGERS, ELLY MZOZO AKIULIZA SWALI |
Timu 64 zitashiriki
michuano hiyo kwa mtindo wa mtoano.
Sehemu ya udhamini
inaonyesha kuwa bingwa wa mashindano hayo atabeba kitita cha Sh milioni 50 na
wakati wa safari kucheza ugenini timu itapata Sh milioni 3 huku mwenyeji akipa
Sh milioni moja. Kumbuka mechi zitapigwa nyumbani na ugenini.
Akizungumza katika halfa fupi
ya mkataba huo kwenye Ukumbi wa mikutano wa Jengo la Kisenga LAPF, Kijitonyama
jijinai , Dar es Salaam, Rais wa TFF, Jamal Malinzi, amesema:
Malinzi amesema kwamba
duniani kote maendeleo ya soka yanatokana na kuwepo na mashindano mbalimbali
yakiwemo ya Kombe la Shirikisho la nchi, ambayo yanashirikisha na klabu za
chini hadi zile zinazoshiriki Ligi Kuu.
“Udhamini huu utachangia soka kukua kwa kiasi kikubwa, nashukuru sana kuona mambo yamefikia hapa, ahsante kwa Azam Media kwa uamuzi wao wa kuingia kukuza mpira wa Tanzania,” alisema Malinzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment