Kiatu cha mshambuliaji
mpya wa Simba, Pape Ndaw raia Senegal kimekuwa gumzo kupita kiasi mitandaoni.
Mshambuliaji huyo
aliingia katika mechi hiyo kuchukua nafasi ya Hassan Kessy wakati Simba ikiivaa
Yanga na kupoteza kwa mabao 2-0.
Ndaw ambaye urefu wake ni
futi 6.6 na ndiye mchezaji mrefu zaidi katika Ligi Kuu Bara, alionekana akiwa
amevaa kiatu aina ya Adidas chenye rangi nyeupe na bluu kikiwa kimechakaa
kwelikweli.
Kiatu hicho ‘kilivutwa’
na runinga ya Azam TV na kuzua gumzo kwelikweli.
Uchakavu wa kiatu hicho
ambacho ukubwa wake utakuwa zaidi ya namba 12, kilionekana kuchoka utafikiri
wachezaji wa ‘mchangani’.
Kuanzia hapo, mashabiki
wa Yanga wameanza kuwadhihaki wenzao wa Simba kwamba wamesajili mchezaji ambaye
hana hata fedha ya kununua kiatu tu!
Wengi walikuwa
wakiwatania Simba na kuwaambia ‘wamepigwa’ hawezi kuwa ana mawasiliano au
mkataba na Steau Bucharest ya Romania wakati hata kiasi tu hawezi kununua tena
katika mechi kubwa kama hiyo.
Baadhi ya mashabiki wa
Simba walikuwa wakijibu mapigo kwamba kununua kiatu si kazi ya klabu, badala
yake mchezaji mwenyewe.
0 COMMENTS:
Post a Comment