Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetuma
salam za rambirambi kwa mwenyekiti wa klabu ya Coastal Union, Dr Twaha Ahmed
kufuatia kifo cha mchezaji Mshauri Salim aliyefariki jana jioni jijini Tanga.
Katika salam hizo za Rais wa TFF Jamal Malinzi kwenda
kwa uongozi wa klabu ya Coastal Union, amewapa pole wafiwa ndugu jamaa na
marafiki pamoja na uongozi wa klabu hiyo na kusema TFF wako nao pamoja katika
kipindi hichi cha maombelezo.
Marehemu Mshauri Salim alikuwa mchezaji wa kikosi cha
vijana (U20) cha Coastal Union, alifariki jana jioni wakati akipelekwa
hospitali baada ya kuanguka uwanjani wakati wa mchezo wa utangulizi wa timu
yake dhidi ya timu ya Eagle Academy ya jiji humo.
Kabla ya umauti kumfika, Mshauri aligongana na
mchezaji wa timu ya Eagle Academy na kutolewa nje kwa matibabu, ambapo aliweza
kurudi uwanjani na kuendelea na mchezo huo kabla ya kuanguka peke yake tena
uwanjani na kufariki akiwa njiani kupelekwa hospitalini.
0 COMMENTS:
Post a Comment