September 26, 2015


MPIRA UMEKISHAAAAAAAAA
DK 90+8, Twite anapewa kadi ya pili ya njano, inazaa kadi nyekundu
Dk 90+2 hadi 90+6, Simba wanaonekana kushambulia zaidi, lakini hakuna lolote wanalofanya kutokana na kuonekana wana presha kubwa

Dk 90+1, Barthez analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda. Hii ni kadi ya tano ya njano kwa Yanga wakati Simba wanazo nne.



Dk 90+7
(Mwamuzi anainua ubao kuonyesha dakika 7 za nyongeza

Dk 89, Kiiza anaingia anajaribu kuuwahi mpira lakini barthez anauwahi na hapohapo anajilaza kupoteza muda

Dk 88, nafasi nzuri kuliko zote, Awadhi Juma akiwa na lango lililo wazi, anapiga mpira juu hukukipa akiwa [embeni ya lango
SUB: DK 87, Yanga wanamtoa Tambwe anaingia Deus Kaseke
SUB: Dk 84, Simba wanamtoa Kessy anaingia mchezaji mrefu kuliko wote Ligi Kuu Bara, Pape Ndawa raia wa Senegal

SUB Dk 82, Yanga wanamtoa Telela na nafasi yake anaingia Said Juma 'Makapu' ili kuongeza nguvu katika kiungo cha ukabaji



Dk 81, Kiiza anaingia eneo la hatari na kupiga shuti lakini ni goal kichk
KADI: Dk 80, Busungu analambwa kadi ya njano kutokana na kuvua jezi wakati akishangilia
GOOOOOOOOOOO Dk 79, Busungu anaipatia Yanga bao la pili saaaafi kabisa. Ulikuwa mpira wa kurushwa wa Mbuyu Twite lakini akauparaza Tambwe, na kumkuta mfungaji ambaye akapiga kichwa kwa ulaini mbele ya Kessy na kuandika bao
Dk 78, Ngoma anamkibiza Isihaka anatoa mpira, inachongwa kona na Niyonzima, anaokoa Isihaka mwenyewe

Dk 76, krosi safi ya Niyonzima, Ngoma anaruka juu na kupiga kichwa vizuri kabisa. Lakini unapita juuuu

KADI: Dk 75, Kessy analambwa kadi ya njano kwa kumkata ngwara Ngoma

Dk 73 Yanga wanapata nafasi nzuri sana, Tambwe anaingia aeneo la hatari lakini anashindwa kutoa pasi nzuri kwa Ngoma
Dk 69 kunazuka tafrani kidogo baada ya wachezaji kutaka kuanza kupigana, Ngoma anadai kuumizwa, lakini akiwa nchini anampiga mchezaji mmoja wa Simba kwa mkono, wengine wanaingilia kuamua na inaonekana kama kuna mmoja wao alimkanyaga Ngoma akiwa chini, hivyo kusababisha ainuke kwa jazba

KADI: Dk 67 Mwamuzi Nkongo anatoa kadi ya njano kwa Tshabalala baada ya kumuangusha Busungu

KADI: Dk 64 Twite analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Tshabalala

SUB: Dk 62, Simba inamtoa nahodha wao Mgosi na nafasi yake inachukuliwa na kinda Ibrahim Ajibu

Dk 59, Barthez anaanguka akisema amegongwa na Kiiza. Hata hivyo inaonekana hakuwa ameguswa kwa nguvu sana. Sasa mpira umesimama anatibiwa

Dk 56 Kamusoko anapiga vizuri lakini mpira unawababatiza mabeki wa Simba na kumkuta Mwinyi anapiga hvyo na kuwagoal kick

Dk 55, Majabvi anamuangusha Busungu na mwamuzi anasema ni faulo, kama mita 28 au 30 nje ya lango la Sima, anapiga Kamusoko
Dk 53, Ngoma anamtoka Isihaka kwa chenga ya 'tangulia naja', lakini anamwangusha na mwamuzi anamuita kumuonya kwa mdomo



Dk 52, krosi safi ya Telela lakini inakosa mwenyewe na Simba wanajitokeza na kuokoa
DK 49, Kazimoto anapicha chenga nzuri ndani ya boksi, lakini shuti lake linakuwa kuuubwaaaa

Dk 46, Ngoma anajaribu kumtoka Juuko, lakini anauwahi mpira na kuondosha hatari


(SIMBA WAMEMALIZA KIPINDI CHA KWANZA WAKIWA NA 51% KUMILIKI YA YANGA 49%, Mashuti moja kwa kila timu huku Simba wakipiga matano bila kulenga lango na Yanga matatu ambayo hayakulenga pia)

MAPUMZIKOOO
Dk 45+2
GOOOOOOO Dk 44, Tambwe anafunga bao safi la kiufundi katikati ya mabeki watatu wa Simba lakini anapiga na mpira unajaa wavuni
 Dk 42, Ngoma anajaribu kumtoka Isihaka lakini anauwahi mpira na kuutoa, kona, inachongwa na Niyonzima na Manyika anaidaka kwa madaha kabisa kama nyani

Dk 41 Manyika anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti la Tambwe inakuwa kona inayochongwa na Niyonzima lakini haina madhara

Dk 38 hadi 40 mpira zaidi unacheza katikati ya uwanja
Dk 37, nafasi nyingine nzuri kwa Simba, Kiiza anawawahi mabeki wa Yanga na kupiga kichwa safi sana lakini unapiga juu kidogo tu

KADI Dk 36, Mgosi na Telela wanalambwa kadi ya njano kila mmoja kutokana na kufanya madhambi kwa wakati tofauti

SUB: Dk 34, Yanga wanafanya mabadiliko ya kwanza ya mchezo huu, Wanamtoa Msuva na nafasi yake inachukuliwa na Malimi Busungu

Dk 32, mpira upo katikati zaidi, hakuna timu imeshambulia hadi sasa. Kamusoko ana Niyonzima wanaonekana kugongeana bila ya kwenda mbele tofauti na Kazimoto na Ndemla wa Simba ambao wanapeleka amshambulizi mengi zaidi

Dk 30, Mgosi anaruka na kuupiga mpira lakini unapita juu na kuwa goal kick

Dk 28, Kiiza ndani ya eneo la hatari baada ya pasi ya Kazimoto, anapiga shuti safi lakini Barthez anafanya kazi ya ziada kuokoa na kuwa kona. Hii ndiyo nafasi nzuri zaidi ya mchezo hadi sasa

Dk 26, mwamuzi wa akiba anafanya 'blanda', mpira anautoa Tambwe, yeye anasema kona ipigwe kuelekea lango la Simba.
Dk 24, pasi nzuri ya Kazimoto, Kiiza anapiga krosi lakini Cannavaro anaokoa na kuwa kona isiyo na faida



Dk 22, Haji Mwinyi naye anakuwa wa kwanza kujaribu kwenye lango la Simba, lakini shuti dhaifu
Dk 21, Tshabalala anapiga shuti la kwanza langoni, lakini ni dhaifu, linatoka na kuwa goal kick

Dk 16 hadi 19, mpira unaonekana kuchezwa katika zaidi huku hakuna hata shuti moja kutoka kwenye lango la timu yoyote.
Dk 14, Kessy anaanguka baada ya kupigwa kichwa kwa makusudi na Ngoma, lakini mwamuzi hakuona

Dk 13, Simba wanafanya shambulizi kali sana, pasi nzuri ya Mgosi, Kiiza anaingia lakini Yondani anawahi, hata hivyo anagongana na kipa wake Barthez, hata hivyo anafanikiwa kuokoa

KADI Dk 12, Juuko analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Ngoma

Dk 9, Simba wanafanya shambulizi zuri baada ya Kazimoto kugongeka vizuri ana Ndemla lakini mpira anaopiga unatoka kidogo nje ya lango
Dk 7, Barthez anarejea tena baada ya matibabu, anainuka na mechi inaendelea
Dk 5 kona nzuri ya Awadhi Juma inaingia katikati ya lango lakini Barthez anauwahi na kudaka. Hata hivyo anaumia na sasa anatbiwa
Dk 4, anaingia na kupiga krosi nzuri, lakini Yondani anafanya kazi ya ziada kuokoa inakuwa kona

Mechi imeanza, Simba imefanikiwa kushambulia mara moja na Yanga mara moja na mpira unachezwa katikati zaidi.
SIMBA....
1. Peter Manyika
2. Hassan Kessy
3. Mohammed Hussein Tshabalala
4. Hassan Isihaka
5. Juuko Murshid
6. Justice Majabvi
7. Mwinyi Kazimoto
 8. Said Ndemla
9. Hamis Kiiza
10. Mussa Mgosi

 11.Awadh Juma

YANGA....
Ally Mustapha ‘Barthez’
Mbuyu Twite
Mwinyi Haji
Nadir Haroub ‘Cannavaro’
Kelvin Yondani
Said Juma ‘Makapu’
Saimon Msuva
Thabani Kamusoko
Amissi Tambwe
Donald Ngoma
Haruna Niyonzima

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic