Kikosi cha Majimaji ya Songea kimeendeleza vipigo baada ya
kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wageni wake Kagera Sugar.
Licha ya Kagera Sugar kuanza ligi hiyo na ushindi wa bao 1-0
wakiwa ugenini dhidi ya Mbeya City, leo mambo yamekuwa tofauti.
Mechi yake ya kwanza ikiwa imerejea Ligi Kuu Bara, Majimaji iliibuka JKT Ruvu.
Mechi ilikuwa ngumu na kila upande ukishambulia kwa zamu, lakini
mwisho mashujaa walikuwa ni Majimaji waliokuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.
Ushindi huo unaifanya Majimaji kuwa timu pekee iliyopanda daraja msimu huu katika nne kufikisha pointi 6 katika mechi mbili za mwanzo za ligi.
Timu nyingine zilizopanda daraja ni Toto, Mwadui FC na African Sports ya Tanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment