MASHABIKI WA ROYAL EAGLES YA JIJINI DARBUN NCHINI AFRIKA KUSINI... |
Mshambuliaji Uhuru Selemani amekuwa kivutio kikubwa kwa
mashabiki wa Royal Eagles ya Afrika Kusini.
Uhuru ambaye amejiunga na timu hiyo ya daraja la kwanza,
akipelekwa kwa mkopo na Jomo Cosmos inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini amekuwa
gumzo kwa mashabiki wa soka nchini wa klabu hiyo.
“Tulikuwa uwanjani katika mechi dhidi ya Santos, Uhuru
alifunga bao la nne na mashabiki wanaume kwa wanawake wakaanza kushangilia kwa
nguvu.
“Hawakuwa wakiimba Uhuru, badala yake walikuwa wakisema
Mwambungu kwa kuwa ndiyo jina analotumia katika jezi yake,” alisema Thomas
Heri, Mtanzania anayeishi nchini Afrika Kusini.
Uhuru alifunga bao la nne wakati Santos ikilala kwa bao 4-1
dhidi ya timu yake hiyo.
Hilo lilikuwa bao lake la pili baada ya kufunga moja katika
mechi yake ya kwanza alipoingoza Royal Eagles kuibuka na ushindi wa bao 2-1
dhidi ya Amazulu.
asanteni kwa yote
ReplyDelete