KIKOSI CHA MBEYA CITY MSIMU ULIOPITA. |
Zikiwa zimebaki siku nne kabla ya kipenga cha Ligi Kuu Bara kuanza
kutimua vumbi, uongozi wa Mbeya City umefunguka kuwa unahitaji kuanza kupata
pointi tatu kuanzia mchezo wa kwanza mpaka msimu unapomalizika.
Utakuwa msimu wa tatu kwa timu hiyo ambayo safari hii itaanzia
tena nyumbani kama misimu miwili iliyopita licha ya kushindwa kuondoka na
ushindi na kuambulia sare mara mbili.
Msimu wa kwanza wa mwaka 2013/14 walifungua dhidi ya Kagera
Sugar na walitoka sare 0-0, msimu uliofuata dhidi ya JKT Ruvu 0-0 kwenye uwanja
huohuo na safari hii wanafungua kwa mara nyingine na Kagera Sugar.
Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, alifunguka kuwa,
wanaanza nyumbani lakini wao wamejipanga kwa ajili ya msimu mzima na wamepania kuanza
kuondoka na pointi tatu katika mchezo wa kwanza.
Kimbe alisema kuwa kikosi
chao msimu huu kimefanya usajili wa uhakika, ingawa timu hiyo itakuwa na
mabadiliko.
“Malengo yetu ni kufanya vyema zaidi msimu huu, ingawa ni wazi
ushindani utakuwa mkubwa lakini upande wetu tunahitaji Mbeya City ianze
kuchukua pointi tatu kuanzia mchezo wa kwanza mpaka wa mwisho bila kujali
inacheza na nani.
“Misimu miwili mechi za ufunguzi hatujaondoka na pointi tatu na
kucheza na Kagera kwa mara ya pili kwenye ufunguzi si tatizo, sisi zaidi
tunaangalia jinsi ya kupambana na kuweza kufikia malengo,” alisema Kimbe.
0 COMMENTS:
Post a Comment