MAREHEMU MSHAURI IDDI |
Coastal Union imepata
msiba baada ya mchezaji wake wa timu ya vijana chini ya miaka 20 kufariki dunia
uwanjani.
Mshauri Iddi amefariki
duniani Uwanjani wakati alipogongana na mwenzake kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Alikuwa akicheza mechi ya
utangulizi za vijana chini ya miaka 20 dhidi ya Coastal Union.
Baadaye Coastal Union ya
wakubwa ilitoka sare ya bila kufungana na Mwadui FC inayofundishwa na Jamhuri
Kihwelo ‘Julio’ aliyewahi pia kuifundisha timu hiyo.
Juhudi kubwa zilifanyika
kujaribu kuokoa maisha yake ikiwa ni pamoja na kumkimbiza hospitali lakini
ilishindikana.
0 COMMENTS:
Post a Comment