Kocha
Mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ametamba kuwa, kama haki itapewa nafasi
katika Ligi Kuu Bara, timu yake itafanya maajabu na inaweza kubeba hata
ubingwa.
Kihwelo
ambaye ni maarufu kama Julio amesema Mwadui FC chini yake ina uwezo mkubwa wa
kubeba ubingwa.
“Tofauti
na wengi wanavyofikiri, Mwadui inaweza kubeba ubingwa. Kwao ni maajabu lakini
kwetu inawezekana.
“Tunachotaka
ni haki ifuate mkondo wake, kama itakuwa hivyo tutawashangaza wengi sana,”
alisema Julio.
Mwadui
FC ambayo imepanda ligi kuu msimu huu, inaanza leo kucheza na Toto African
ikiwa ugenini mjini Mwanza.
Msimu
uliopita, Mwadui FC ilipanda pia kwa wingi wa pointi, lakini mwishoni Stand
United ya Shinyanga pia ikashinda rufaa na kuchukua nafasi ya Mwadui FC.







0 COMMENTS:
Post a Comment