SAMATTA |
Wachezaji watatu wa kimataifa wa Tanzania wanacheza
soka la kulipwa nje ya nchi, Mrisho Ngasa (Free State – Afrika Kusini) Thomas
Ulimwengu na Mbwana Samatta (TP Mazembe – Congo DRC) wamejiunga na kambi ya
Taifa Stars iliyopo katika hoteli ya Urban Rose – Kisutu jana jijini Dar es
salaam.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars Charels Mkwasa amewapokea
wachezaji hao na jana kufanya mazoezi pamoja na wachezaji waliokuwa kambini
nchini Uturuki saa 10 jioni katika uwanja Taifa jijini Dar salaam.
Kwa mujibu wa ratiba ya kocha Mkwasa Stars leo alhamis
itaendelea na mazoezi jioni saa 10 katika uwanja wa Taifa kabla ya kufanya
mazoezi mepesi ya mwisho kesho ijumaa asubuhi.
Wachezaji waliopo kambini ni magolikipa Ally Mustafa,
Said Mohamed, walinzi Juma Abdul, Shomari Kapombe, Haji Mwinyi, Mohamed
Hussein, Kelvin Yondani, Hassan Isihaka na nahodha Nadri Haroub “Cannavaro”.
Viungo ni Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya,
Said Ndemla, Salum Telela, Deus Kaseke, Saimon Msuva na Farid Musa, huku safu
ya ushambuliaji ikiwa na John Bocco, Rashid Mandawa, Ibrahim Ajib, Thomas
Ulimwengu, Mrisho Ngasa na Mbwana Samatta.
0 COMMENTS:
Post a Comment