Maandalizi ya mchezo kati ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Nigeria
(Super Eagles) yamekamilika, ambapo leo Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini
(TFF) limetangaza viingilio vya mchezo huo wa jumamosi kati huku kiingilio cha
chini kabisa kikiwa shilingi elfu saba tu.
Viingilio vya mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya
Afrika (AFCON Qaulifier 2017) kundi G itakua ni VIP A Tsh 40,000, VIP B Tsh
30,000, VIP C Tsh15,000, Rangi ya Machungwa (Orange) Tsh 10,000, na viti vya
rangi ya Bluu na Kijani Tsh 7,000.
Tiketi za mchezo huo zinatarajiwa kuanza kuuzwa kesho siku ya ijumaa saa
4 kamili asubuhi katika vituo kumi vifuatavyo:
(i) Ofisi za TFF - Karume
(ii) Buguruni – Oilcom
(iii) Mbagala – Dar live
(iv) Ubungo – Oilcom
(v) Makumbusho – Stendi
(vi) Uwanja wa Taifa
(vii) Mwenge – Stendi
(viii) Kivukoni- Feri
(ix) Posta – Luther House
(x) Big Bon – Msimbazi Kariakooo
TFF inawaomba watanzania, wapenzi na wadau wa mpira wa miguu kununua
tiketi za mchezo huo katika magari yaliyopo kwenye vituo vilivyotajwa ili
kuondokana na tatizo la kuuziwa tiketi zisizokuwa halali.
Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na idara nyingine za kiusalama
wameandaa usalama wa kutosha katika kuelekea kwenye mchezo na kuhakikisha kila
mpenzi wa mpira wa miguu anaingia kushuhudia mchezo huo salama na kuondoka
salama.
Mchezo huo utaanza saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki
utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Rwanda ambao wanatarajiwa kuwasili leo
jioni pamoja na kamisaa wa mchezo huo.
Waamuzi wa mchezo huo ni Louis Hakizimana (mwamuzi wa kati) Honore Simba
(mwamuzi msaidizi), Jean Bosco Niyitegeka (mwamuzi msaidizi), Abdoul Karim
Twagiramukiza (mwamuzi wa akiba) wote kutoka Rwanda na kamisaaa ni Charles
Kasembe kutoka nchini Uganda.
0 COMMENTS:
Post a Comment