Timu kibonde ya Molde ya nchini Norway imewatwanga
Fenerbahce kwa mabao 3-1 katika mechi ya ufunguzi wa Kundi A ligi ya Europa.
Kipigo hicho cha kushitua kwa timu hiyo kongwe nchini
Uturuki, tena ikiwa na nyota kama Robin van Persie na nani, kimeonyesha
kuwashangaza wengi.
Licha ya kuwa nyumbani, huku ikipata bao la Luis Nani, bado
ilishindwa kujirekebisha.
Bado mchezaji mmoja wa Molde alilambwa kadi nyekundu lakini
bado mastaa hao walishindwa kuikomboa timu yao.
0 COMMENTS:
Post a Comment