Timu ya soka ya taifa
ya Wanawake, Twiga Stars imeanza michezo ya All African Games kwa kupoteza kwa
bao 1-0 dhidi ya Ivory Coast.
Licha kusafiri kwa ‘kuungaunga’,
lakini Twiga Stars imefanikiwa kuonyesha kiwango lakini mwisho ikapoteza kwa
bao hilo moja.
Michuano hiyo ya All
African Games inafanyika nchini Congo katika jiji la Brazaville.
Ivory Coast ni moja ya timu bora za wanawake katika bara la Afrika na ilipata maandalizi ya kutosha.
Kwa viwango vya Fifa, Ivory Coast inashika namba 67 huku ikishika nafasi ya 6 kwa viwango vya Fifa, huku Tanzania kupitia Twiga Stars ikiwa katika nafasi ya 129.
Ukiachana na Ivory Coast, Twiga bado ina kibarua kigumu kwa kuwa itakutana na Nigeria na wenyeji Congo ambao wako kundi moja.
Jumatano itakuwa mechi yao ya pili dhidi ya Nigeria, kabla ya Jumamosi kukutana na wenyeji Congo.

0 COMMENTS:
Post a Comment