![]() |
| PICHA YA SIMU ILIYOPIGWA YANGA WAKIFANYA MAZOEZI MJINI PEMBA |
Yanga wako mjini Pemba, tayari wameanza mazoezi kujiwinda na mechi yao
ya Jumamos dhidi ya watani wao Simba ambao wako mjini Zanzibar.
Kikosi cha Yanga, tayari kimeanza mazoezi kwenye Uwanja wa Gombani, lakini ajabu, hawataki kupigwa picha.
Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amewaambia waandishi kwamba haitakiwi
kupiga picha mazoezi.
“Haya ni maelekezo ya uongozi, hivyo hatutazungumza wala hatutaki
picha,” alisema Hafidhi.
Hata hivyo, waandishi walipinga hilo na kuwataka Yanga kuwapa nafasi ya
kufanya kazi yao.
Jambo hilo lilizua mzozo kati ya kiongozi huyo na waandishi huku mashabiki
wakitaka waandishi wapewe nafasi ili Wanayanga wajue timu yao inaendeleaje kwa
kuwa sasa iko mbali na sehemu kubwa ya Tanzania wanataka kujua inaendeleaje.








0 COMMENTS:
Post a Comment