Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluim
amewataka wachezaji kusahau kabisa kuhusiana na suala la mabao 5-0 waliyofungwa
na Simba.
Akizungumza kutoka mjini Chake Chake,
Pluijm ameitaka Yanga kusahau kipigo hicho cha Simba ili wagange yajayo.
“Kufungwa katika soka ni jambo la
kawaida kabisa. Huu ndiyo wakati wachezaji wanapaswa kusahau yale masuala ya
kipigo hicho.
“Ukitaka kuwafunga Simba, kwanza lazima
usahau kipigo cha mabao matano. La sivyo tutaendelea kubaki hapa,” alisema.
Pluijm na Yanga wako mjini Chake Chake
kisiwani Pemba kujiandaa na mechi dhidi ya watani wake Simba.
Mechi hiyo ya watani itakayopigwa
Jumamosi, inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi tena kwa hamu kubwa.
Simba imejichimbia mjini Unguja kwa
ajili ya mechi hiyo pia ambayo kila timu inataka kuendeleza ushindi baada ya
kuanza na ushindi katika mechi zote tatu za mwanzo.
Tayari Yanga wameanza kujifua kwenye Uwanja wa Gombani







0 COMMENTS:
Post a Comment