October 8, 2015

NIMUBONA KATIKA MAZOEZI YA SIMBA LEO
Beki Emiry Nimubona atakuwa nje ya kikosi chake cha Simba kwa wiki nne.


Nimubona amevunjika mmoja wa mfupa mdogo wa mkono wake na sasa amefungwa bandeji ngumu maarufu POP.

Beki huyo raia wa Burundi, leo alifanya mazoezi na wenzake, lakini baadaye akaanza kusikia maumivu makali na kulazimika kupelekwa hospitali.

“Kweli alisikia maumivu makali, akapelekwa hospitali wakagundua kwamba alivunjika mfupa ambao unakwenda kwenye kidole.


“Aliwahi kuvunji hiyo sehemu, huenda hakujua safari hii kwamba maumivu yake ni tatizo hilo. Baada ya kufika hospitali wakagundua kuwa ni tatizo hilo,” kilieleza chanzo.

Kuhusiana na taarifa hivyo, Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Simba, Haji Manara amethibitisha na kusema tayari amepokea taarifa hizo.

"Kweli amewekewa POP, sasa atakuwa nje kwa mwezi mzima," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic