Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Jumatano kati ya Tanzania (Taifa
Stars) dhidi ya Malawi (The Flames) kuwa ni shilingi elfu kumi tu (10,000)
katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia mwaka 2018
nchini Urusi.
Viingilio vilivyotangazwa leo ni
kiingilio cha juu kabisa kwa mchezo huo shilingi elfu kumi (10,000) kwa viti
vya VIP B & C, huku viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani ikiwa ni
shilingi elfu tano (5,000).
Stars inayonolewa na kocha mzawa Charles
Boniface Mkwasa imeendelea kujifua katika viwanja vya Gymkhana na uwanja Taifa
jioni kujiandaa mchezo huo wa Jumatano dhidi ya Malawi, huku wachezaji wakiwa
wenye ari na morali ya hali ya juu kuelekea kwenye mechi hiyo.
Wachezaji 22 wapo kambini akiwemo
mshambuliaji Mrisho Ngasa anayecheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini
aliyeripoti jana mchana kambini, huku wachezaji wawili Mbwana Samata na Thomas
Ulimwengu wakitarajiwa kujiunga na wenzao leo wakitokea Lubumbashi – Congo DR.
Wakati huo huo timu ya Taifa ya Malawi (The
Flames) imewasili nchini jana saa 4 asubuhi na kufikia katika hoteli ya De Mag
iliyopo Mwanayamala, ambapo kikosi hicho leo kimefanya mazoezi asubuhi katika
uwanja wa Boko Veterani.
Waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini
Somalia, kamisaa na mtathimin waamuzi wa wanatarajiwa kuwasili leo nchini na
kufikia katika hoteli ya Protea iliyopo Oysterbay.
Mwamuzi wa kati ni Hagi Yabarow Wiish
(Somalia), akisaidiwa na Hamza Hagi Abdi (Somalia), Salah Omar Abubakar
(Somalia), mwamuzi wa akiba Bashir Olad Arab (Somalia), mtathimini wa waamuzi
Sam Essam Islam (Misri) na kamisaa wa mchezo ni Muzambi Gladmore (Zimbabwe).
0 COMMENTS:
Post a Comment