October 19, 2015


Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr, amesema licha ya kutowafahamu vizuri wapinzani wake katika mechi ya keshokutwa Jumatano, Tanzania Prisons ya Mbeya, bado anaamini timu yake itaibuka na ushindi.


Timu hizo zitakutana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara mkoani hapa, ambapo Simba imekuwa ikipata wakati mgumu kila inapokuja Mbeya kucheza, lakini kitendo cha kuifunga Mbeya City, juzi kimemuongezea morali ya kushinda katika kipute dhidi ya Prisons.

Mara tu baada ya mechi dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine ambapo pia ndipo kutakapofanyika mchezo wa keshokutwa, Kerr raia wa Uingereza alisema hawafahamu wapinzani wake lakini amekuwa akiambiwa wana timu ngumu.

“Nimeambiwa Prisons ni timu ngumu kwa Simba, lakini sina wasiwasi wowote, timu yangu ipo fiti na wachezaji wanaonyesha kuzoeana na tumeshazoea mazingira ya Mbeya,” alisema Kerr.

Alisema hakuna kinachoshindikana na lengo lao ni kuibuka na ushindi tu katika mchezo huo.


“Mbeya City wao tuliwaona kabla ya mchezo tukawajua mapema aina ya uchezaji wao, hivyo tutahakikisha tunavuna pointi zote sita licha ya mimi binafsi kutowajua Prisons,” alisema Kerr.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic