October 7, 2015

MBEYA CITY

Kocha Mkuu wa Simba Muingereza, Dylan Kerr, amewataka wachezaji wake kuhakikisha wanajituma na kufanya mazoezi kwa nguvu zote ili kuimarisha viwango vyao ili waifunge Mbeya City na kudai kuwa mchezo huo utakuwa mgumu.


Mbeya City na Simba zinatarajiwa kukutana Oktoba 17, mwaka huu katika Dimba la Sokoine jijini Mbeya, ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa saba wa Ligi Kuu Bara.

Kerr amesema ili timu yake iweze kufanikiwa kufanya vizuri katika mchezo dhidi ya Mbeya City na michezo ijayo, wanatakiwa kujituma katika mazoezi ili kikosi kiweze kuwa imara zaidi.


“Mechi ya Mbeya City itakuwa ngumu kwa kuwa kila mchezo tunaocheza unakuwa na ushindani kwani kila timu inataka kuifunga Simba, hivyo wachezaji wanahitaji kujituma ili kufanya vizuri.

“Ligi ni ngumu kila timu inahitaji kufanya vizuri, hivyo tuna siku 15 kabla ya kukutana na Mbeya City ni vyema nikawapa mazoezi imara na ya kujenga stamina ili kushinda  mchezo huo, jambo la msingi hapa ni kupata pointi tatu.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic