October 14, 2015


Straika nyota wa Simba, Mganda, Hamis Kiiza, amejitoa kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachoivaa Mbeya City katika mechi ya Ligi Kuu Bara, wikiendi hii.

Mganda huyo, amejitoa kwenye kikosi hicho kutokana majeraha ya nyama za paja zinazomuuma baada ya kuumia wiki iliyopita katika mazoezi ya timu hiyo.

Kutokana na majeraha hayo, mshambuliaji huyo alishauriwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki mbili na daktari mkuu wa timu hiyo, Yassin Gembe, katika kipindi hicho alitakiwa kupumzika wiki moja kabla ya wiki ya pili kuanza mazoezi.

Kiiza alisema kuwa kwa mujibu wa programu aliyopewa juzi Jumatatu, alitakiwa kuanza mazoezi mepesi, lakini imeshindikana kutokana na maumivu anayoyasikia.

 “Uwezekano wa mimi kucheza mechi na Mbeya City ni mdogo, hiyo ni kutokana na kushindwa kuanza mazoezi mepesi niliyotakiwa kuanza kuyafanya jana (juzi) Jumatatu.

“Nimechelewa kuanza mazoezi mepesi kutokana na maumivu ninayoendelea kuyasikia kwenye nyama zangu za paja.

“Kuchelewa huko kurejea uwanjani kumenifanya nishindwe kuamini kama nitacheza mechi inayofuata,” alisema Kiiza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic