October 20, 2015


Kocha Luis Enrique wa Barcelona amesema wanafanya kazi ya ziada kuboresha safu yao ya ulinzi.


Enrique amesema benchi la ufundi wanafanya kazi hiyo na itakuwa inaboreshwa kila wanavyoendelea kucheza.
“Kuna mechi kadhaa tulionyesha kuwa tuna matatizo katika safu ya ulinzi. Sasa tunataka kulimaliza kabisa hilo tatizo,” alisema Enrique.
“Lakini lazima tuendelee kujifunza na kubadilisha, hatuwezi kubadili kila kitu kwa siku mbili,” alisema.
Barcelona imekuwa ni moja ya timu zilizoruhusu mabao mengi katika mechi zake 10 zilizopita.

Wengi wamekuwa wakimtuhumu beki Gerard Piqeu kushuka kiwango.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic