October 20, 2015



Kiungo Yaya Toure ambaye ni mchezaji bora Afrika, ameendelea kusisitiza kuwa hana raha katika kikosi cha Manchester United.


Toure aliwahi kuzozana na Man City kabla ya kukubaliana na City na baadaye kuendelea kubaki.

Toure ,32, amekuwa akiwaeleza rafiki zake kwamba hayuko katika hali inayompa furaha hata kidogo.

Amekuwa akionekana kutokuwa na furaha ingawa ukimya wake unamfanya aonekane kama yuko katika mazingira ya kawaida.

Katika mahojiano na gazeti namba moja la michezo duniani la L’Equipe, Toure amesema hana raha tokea amefika Man City.
“Nilipokwenda City, watu waliona nimekosea, wakanicheka lakini baadaye tukachukua makombe na kuwa gumzo.

“Ajabu hadi sasa hakuna watu hawaoni tulichofanya na hawaonyeshi kukubali,” alisema.

Hata hivyo Toure hakuweka kila kinachomfanya asiwe na furaha.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic