October 20, 2015


Na Paul Mwakipesile, Mbeya
Pamoja na Simba kuonyesha wanajiamini kabla ya kuivaa Prisons, kesho lakini wazi hofu imetanda.

Kocha Simba, Dylan Kerr ametamba kwamba watawafunga Prisons licha ya kwamba haijui timu hiyo.
Lakini jana mjini hapa kulikuwa na ulinzi mkali katika mazoezi ya Simba na waandishi walikataliwa kuingia.
Pamoja na kufanya kwenye Uwanja wa JKT mjini hapa, viongozi wake wa hapa walizuia waandishi kuingia.

Juhudi za waandishi angalau kutaka kupiga picha tu ziligonga mwamba, ikionyesha wazi Simba walikuwa na hofu kuhusiana na Prisons.
Prisons itashuka kwenye Uwanja wa Sokoine kesho ikiwa na hasira ya kupokea kipigo cha mabao 3-0 ugenini mjini Shinyanga dhidi ya Stand United katika mechi yake ya mwisho ya Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic