October 11, 2015


MPIRA UMEKWISHAAAA
KADI 90+3 Chiyasa analambwa kadi ya njano kwa lkumuangisha Ulimwengu


KADI DK 90+2, Samatta naye analambwa kadi ya njano kadi ya njano kwa kukataa kupanda kwenye machela

DAKIKA 9-+4
Dk 89 Mhone anapiga shuti kali linambabatiza Cannavaro na kutoka nje, kona lakini haijazaa matunda

KADI Dk 84 Ulimwengu analambwa kadi ya njano kwa kuwasukuma wahudumu walioingia uwanjani kumchukua baada ya kuumia

Dk 80, Mhone anawahadaa mabeki wa Stars na kupiga shuti kali kwelikweli, lakini mpiraSUB Dk 75 Ngassa anaingia kuchukua nafasi ya Farid

KADI Dk 74, Bocco na Levson Maganizo wanalambwa kadi ya njano kwa kusindikizana

Dk Dk 72, Samatta anapokea pasi ya Bocco, anageuka na kupiga shuti kali lakini goal Kick

Dk 64 hadi 68, Stars wanafanikiwa kutuliza kasi ya Malawi kwa kucheza mpira wa taratibu na kuwabana.

Dk 61, Malawi wanazidisha mashambulizi, Kayira aliyefunga bao kipindi cha kwanza anapiga shuti kali sana

Dk 57 Kayira anapiga shuti kali nje ya 18 lakini Barthez anafanya kazi ya ziada

Dk 53, Samatta anamtoka Fadya na kupiga krosi ahata hivyo inaokolewa

Dk 49 Haji Mwinyi anapiga mpira wa faulo vizuri kabisa lakini kipa anadaka
Dk 47, Kayira anapiga shuti kali lakini anashindwa kulenga lango
SUB Dk 46, anatoka Ndemla na nafasi yake inachukuliwa na John Bocco


MAPUMZIKO
DAKIKA 45+1
KADI Dk 45, Mudathir naye analambwa kadi ya njano kwa kuonyesha ishara ambayo mwamuzo anaona si sahihi


KADI Dk 44 Farid Mussa analambwa kadi ya njano kwa kumvuta John Banda

GOOOOOO Dk 41 John Banda anaifungia Malawi bao la kuongoza baada ya kupiga shuti la kiufundi lililomgonga Yondani mgongoni na kujaaa wavuni

Dk 37, John Banda anaachia shuti kali na hatari, hata anashindwa kulenga lango

Dk 36, Mudathir anapiga shuti kali umbali wa mita 31 hivi, lakini anashindwa kulenga

Dk 35, Ulimwengu la hatari, anapiga shuti linaokolewa na kuwa kona isiyo na matunda

Dk 34, nafasi ya kwanza nzuri kwa Tanzania, Ulimwengu anabaki yeye na lango mbele ya makipa, lakini anashindwa kulenga lango

Dk 32, Malawi wanafanya shambulizi, krosi nzuri ya Chiyasa lakini Barthez kw amara nyingine anafanya kazi ya ziada kuokoa

Dk 26 hadi 31, hakuna timu iliyofanya shambulizi kubwa  mwa wapinzani
Dk 20 hadi 25, Malawi wanaonekana kujipanga zaidi, hata hivyo mpira unachezwa katikati zaidi

Dk 18 Mhone anapiga kichwa akiwa peke yake, lakini Barthez anatulia na kuudaka vizuri kabisa

Dk 15, Himid Mao anapiga shuti la umbali wa mita 33, lakini mpira unapita juu ya lango la Malawi

 Dk 14, Ulimwengu anaangushwa na kuumia, lakini mwamuzi anapeta
Dk 10 Kayira anapiga shuti kali, hatariiiii lakini Barthez anaokoa linagonga mwamba na kurudi uwanjani

Dk 6 Kawanda anaingia ndani ya eneo la hatari, anapiga shuti lakini linambabatiza Yondani na kutoka nje, kona lakini haina matunda

Dk 3, Cannavaro anazubaa, Malawi wanafanikiwa kupata upenyo na kupiga shuti lakini Barthez anafanya kazi ya ziada na kuokoa.


Dk 1, Samatta anafanikiwa kuingia katika eneo la hatari anapiga shuti lakini lake linaokolewa na kipa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic