October 28, 2015

MPIRA UMEKWISHAAAAAADk 90+3
SUB Dk 89, Yanga inamtoa Kamusoko na nafasi yake inachukuliwa na Haruna Niyonzima
 GOOOOOOO Dk 88, Kigodeko anaifungia Mwadui baada kona safi kusababisha piga nikupige na Chuji akatoa pasi kwa mfungaji aliyemalizia vizuri kabisa

Dk 87 Chuji anaingiza mpira mzuri wa juu, purukushani inatokea katika lango la Mwadui. Yanga wanaokoa, konaaa.
Dk 81 hadi 85, Yanga wanaonekana kupoteza muda huku MWadui FC wakiwa na hamu kubwa ya kutaka kupata bao la kusawazisha


Dk 80, Mwadui wanaendelea kusukuma mashambuliz lakini shuti la Bakari Kigodeko linapaa juuu

SUB Dk 75 Athumani Iddi 'Chuji' anaingia kuchukua nafasi ya Semwanza aliyeumia

GOOOOOO Dk 74, Ngoma anaingia ndani ya eneo la hatari huku akimburuza Mgeveke kabla ya kufunga bao kwa ulaini kabisa

Dk 73, Kado anafanya kazi ya ziada na kudaka mpira kichwani mwa Tambwe

SUB Dk 71 Anatoka Tegete kwa upande wa Mwadui anaingia Gwange
KADI Dk 69 Mnyate naye analambwa kadi ya njano kwa kumuumiza Juma AbdulKADI Dk 68 Ngoma analambwa kadi ya njano kwa kumsukuma Nonga kwa makusudi
Dk 68 Yanga inafanya shambulizi kali, Tambwe anapiga kichwa kinagonga mwamba na kuondolewa

Dk 67, Juma Abdul anachonga krosi safi katika lango la Mwadui, mpira unamkuta Twite katika nafasi nzuri hata hivyo ananawa
Dk 64, Juma Abdul anatoa pasi nzuri kwa Ngoma, hata hivyo mpira unamzidi kasi

SUB Dk 61, Deus Kaseke anaingia kuchukua nafasi ya Malimi Busungu
Dk 60, Luhende anamwangusha Ngoma, mwamuzi Adongo anasema ni faulo ielekezwe Mwadui. Tegete ambaye ni nahodha analalamika. unapigwa mpira wa adhabu lakini Yanga wanashindwa kufunga


KADI Dk 58, Mbuyu Twite analambwa kadi ya njano kutokana na mchezo wa kibabe
Dk 55, Tambwe anatoa pasi nzuri kwa Msuva, anapiga shuti linagonga mwamba na kutoka nje

KADI Dk 51 Adongo anamlima Jabir Aziz Stima kadi ya njano baada ya kumkanyaga makusudi Ngoma

Dk 50 mpira unasimama na mwamuzi Jacob Adongo anamuita mchezaji mmoja wa Mwadui
SUB Dk 48 Coutinho anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Simon Msuva

Dk 46, Yanga wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la MWadui, lakini Mgeveke anaondosha hatari

MPIRA MAPUMZIKODk 45+2
Dk 45m krosi safi ya Ndeule inamfikia Tegete anapiga shuti baiskeli lakini mpira unatoka nje kidogo tu


Dk 45, mpira unachezwa katikati zaidi lakini Yanga wanaonekana kuosha kila mpira

Dk 43, Ngoma na Tambwe wanagongeana vizuri na kuingia eneo la hatari, lakini Mwadui FC wanaokoa

GOOOOOOOOO Dk 40, Nonga anaingia vizuri na kufunga bao safi kwa shuti kali sana. Wachezaji wa Yanga walionekana kuamini alikuwa ameotea

Dk 37, Busungu anaingia kwa kasi, mbele ya Mgeveke anapiga shuti kali lakini Kado anadaka vizuri kabisa

Dk 31, Ngoma anakimbia na kutoa pasi safi kwa Tambwe lakini shuti lake linapita juuuu

KADI Dk 28 Paul Nonga analambwa kadi ya njano kwa kumuangushaMbuyu Twite

Dk 24 hadi 27, zaidi mpira unachezwa katikati ya uwanja, MWadui FC wakicheza pasi za juu na Yanga wakipiga chinichini
Dk 22, krosi nzuri ya Juma Abdul inamkuta Tambwe anaunganisha vizuri lakini mpira unatoka juu kidogo ya lando

Dk 21, Nonga anapiga krosi safi kabisa Tegete anauwahi lakini anashindwa kulenga lango

Dk 19, Coutinho anampa pasi Tambwe lakini anapiga shuti mtoto

Dk 17, Tegete anapata nafasi bora kabisa ya mchezo huu hadi sasa lakini anashindwa kufunga 

Dk 16, Mwadui FC wanapata kona ya kwanza inayochongwa na Ndeule lakini Cannavaro anaokoa vizuri kabisaDk 13, Tegete anamtengenezea Ndeule nafasi nzuri, lakini anashindwa kupiga shuti mpira unatoka nje na kuwa goal kick

Dk 10, Mwadui wanaonekana kupambana kutaka kurudisha bao hilo hata hivyo mashambulizi yao bado ni dhaifu

GOOOOOO Dk 8, Ngomaa anaifungia Yanga bao baada ya kuiwahi pasi safi ya Coutinho na kuwazidi ujanja Mgeveke na Si Mwanza kabla ya kufunga kwa ulaini kabisa

 Dk 7, Coutinho naye anapiga shuti kali la adhabu lakini Kado anaka kwa ustadi mkubwa

Dk 3 Ngoma anamtoka Mgeveke na kupiga shuti kali sana lakini Kado anafanya kazi ya ziada kuokoa na mabeki wanaondoa hatari

Dk 2 Mwadui FC wanakuwa wa kwanza kufanya shambilizi katika lango la Yanga lakini juhudi za Paul Nonga zinakatizwa na Cannavaro anayeokoa.


Kocha Hans van der Pluijm ameamua kuanza na kiungo Andre Coutinho kwa mara ya kwanza, huku Mbuyu Twite akipiga namba sita, namba saba ni Thabani kamusoko na Malimi Busungu anapiga namba nane huku Amissi Tambwe na Donald Ngoma wakiongoza mashambulizi.



Upande wa ulinzi Yanga hawana tofauti kwani moja ni Ally Mustapha Barthez, 2. Juma Abdul, 3. Haji Mwinyi, 4. Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic