October 17, 2015


MPIRA UMEKISHAAAAAAAKADI Dk 90, Kapombe anapigwa kadi ya njano kwa kulazimisha kukaa mbele ya mpira

OKOOOOOOAAAA Dk 88 Kamusoko anapiga lakini Aishi Manula anafanya kazi ya ziada na kuukoa mpira huo

Dk 86 Manula analambwa kadi ya njano huku Wawa akiendelea kumlaumu mwamuzi
PENAAAAAAT Dk 84,  Aishi Manula anamwangusha Msuva na mwamuzi anasema ni penalti

GOOOOOOO Dk 81, Kipre Tchetche anaifungia Azam bao la kusawazisha kwa shuti kali baada ya krosi safi ya Kapombe, kumkuta Farid ambaye anammegea mfungaji kitaalamu kabisa
SUB Dk 79, Said Juma 'Makapu' anaingia kuchukua nafasi ya Twite ambaye ameshindwa kurudi uwanjani baada ya kuumia

Dk 77, Kipre anafanya nzuri na kumpa pasi FArid akiwa na kipa Barthez anamlenga na mpira anaukoa
Dk 74, Twite anaumia, anatolewa nje na madaktari wanafanya kazi ya ziada kumshona
DK 70, mpira wa kurushwa mwa Mwantika unaguswa na kugonga mwamba na kuokolewa

SUB: DK 69, anaingia Frank Domayo anaingia kuchukua nafasi ya Bolou 
SUB: Dk 63, anatoka Wanga nafasi yake inachukuliwa na Kipre Tchetche
Dk 59, Ngoma anafanya jaribio jingine lakini kipa Aishi Manula anafanya kazi ya ziada kuokoa


KADI 52, Himid Mao analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha kwa makusudi Busungu

Dk 46 mpira unaanza lakini kila upande unaonekana kuwa makini kwa kusoma upande mwingine


MAPUMZIKODK 45+3
GOOOOOOOO Dk 45anaiwahi vizuri krosi safi ya Juma Abdul, anaweka kifuani na kupiga shuti safi la kuchupa na kuandikia YAnga bao


Dk 43 Sure Boy anaingia na kutoa pasi lakini inakuwa si nzuri sana, inaokolewa

Dk 38 Busungu anamtoka Wawa na kujaribu kupiga shuti lakini mpira unaokolewa na Mwantika

KADI Dk 36 Yondani analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Bocco kwa makusudi
Dk 34, Yondani anapanda na kumchambua Wawa ambaye anakuwa mjanja na kuuzuia
Dk 31, Aggrey Morris anajaribu kwa kupiga shuti kali linalotoka sentimeta chache nje ya lango la Yanga

Dk 29, Bocco anaruka katikati ya Yondani na Cannavaro na kupiga kichwa safi lakini mpira unatoka na kuwa goal kick

Dk 28, Kapombe anawachambua wachezaji wa tatu na kutoa pasi nzuri kwa Allan Wanga lakini anakuwa ameotea

KADI Dk 24 Sure Boy analambwa kadi ya njano kumuangusha Mbuyu Twite. Hata hivyo mwamuzi alikuwa na haraka kwani hakumuangusha

Dk 24, Farid Mussa anamtoka Juma Abdul, anapiga krosi safi kabisa ambayo Barthez anafanya kazi ya ziada kuiokoa
Dk 19, Wanga anaruka na kupiga mpira wa kichwa kwa kuchupa, lakini unakuwa hauna kasi na Ally Mustapha Mtinge anaudaka kwa ulaini
Dk 11, Ngoma anageuka na kupiga shuti kali, hata hivyo anashindwa kulenga lango

Dk 4 hadi 5, Yanga wanaonekana kukaa vizuri katikati ya uwanja huku Kamusoko akiwa injini na kuwapa kazi kubwa Azam FC ambao wameiacha mtu mmoja tu juu ambaye ni Bocco

Dk ya 1, Azam FC wanaanza kupeleka shambulizi lakini Haji Mwinyi anapiga kichwa na kuokoa na John Bocco anauwahi na kumkanyaka Ngoma kwa bahati mabaya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic