October 10, 2015


Kila kitu kinaenda vizuri kwa Kocha Juma Mwambusi kutua Yanga kumsaidia Hans van Der Pluijm kuifundisha timu hiyo akichukua nafasi ya Charles Mkwasa aliyepata kazi Taifa Stars.


Yanga hadi sasa ina orodha ya makocha kadhaa waliotajwa kumudu kazi iliyokuwa ikifanywa na Mkwasa, lakini taarifa zinasema Mwambusi anayeinoa Mbeya City ndiye mwenye nafasi kubwa ya kupewa dili hilo.

“Pluijm ndiye anayesubiriwa kutoa jibu lake juu ya msaidizi wake na Mwambusi anapewa nafasi kubwa kutokana na uwezo wake hasa jinsi anavyoifunga Simba kila mara,” kilisema chanzo chetu.

Alipotafutwa Katibu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha ili atoe ufafanuzi kuhusu jambo hilo, alisema: “Tuna majina ya makocha wengi na Jumapili (kesho) tutamtangaza aliyekidhi vigezo na Jumatatu ataanza kazi.”

Mwambusi mwenyewe amekuwa mgumu wa kutoa ufafanuzi kuhusu kuhusishwa kwake na Yanga kwani mara kadhaa hapokei simu yake ikidaiwa yupo katika mazungumzo ya kina na viongozi wake.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic