October 10, 2015


Kocha Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’, amesema kama kuna kitu kigumu katika kazi hiyo ni kuifundisha timu mpya katika ligi na sasa kichwa kinamuuma kuifundisha Mwadui FC katika Ligi Kuu Bara.


Ikiwa chini ya Julio, Mwadui ya Shinyanga sasa ipo katika nafasi ya nane ikiwa na pointi nane ikiwa imecheza mechi sita kati ya hizo imeshinda mbili, sare mbili na imefungwa mara mbili.

Julio amesema: “Usione tumepata pointi hizo nane, ni kazi kubwa kuifundisha timu mpya katika ligi, mimi hapa kichwa kinaniuma wakati mwingine.”

Hata hivyo, Mwadui FC imekuwa moja ya timu zinazoonyesha kandanda safi na ushindani wa juu kwa timu nyingine zinazokutana nayo.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic