Unaweza kuona kama miujiza! Straika wa Simba, Pape N’daw,
amekana kukutwa na hirizi na amesema hajawahi kujihusisha na vitendo vya
kishirikina na hata siku moja hawezi kushiriki vitendo hivyo.
Jumatano iliyopita kwenye Uwanja wa Sokoine,
Mbeya akicheza dhidi ya Prisons, N’daw, raia wa Senegal, alizongwa na wachezaji
wa timu pinzani kisha akakutwa na hirizi ambapo mwamuzi alimtoa nje kwenda
kuitoa.
N’daw amesema: “Sikukutwa
na kitu chochote, ndiyo maana umeona nilikuwa nabishana na wale wachezaji, kama
kuna kitu kimeonekana hakinihusu mimi.”
Kwa kosa la kujihusisha na vitendo vya
ushirikina uwanjani, straika wa Simba, Pape N’daw yupo hatarini kupewa adhabu
ya kufungiwa kucheza mechi zisizopungu tatu za Ligi Kuu Bara.
Pia, kwa mujibu wa kanuni namba 37 ya ligi kuu
kipengele cha 7 (e), N’daw atafungiwa kucheza mechi tatu na kupigwa faini ya Sh
500,000 kwa kosa hilo.
Kanuni hiyo inasema kuwa kufanya vitendo vyenye
kuonyesha imani za kishirikina, uchawi adhabu yake itakuwa ni kufungiwa mechi
tatu na faini ya Sh laki tano.
0 COMMENTS:
Post a Comment