October 20, 2015

NSA JOB WAKATI AKIICHEZEA YANGA.

Straika wa zamani wa Yanga, Nsa Job yu amelazwa taabani katika Hospitali KCMC mjini Moshi.

Nsa aliyewahi kuichezea Yanga na Coastal Union amelazwa akiwa taabani baada ya kupigwa jiwe kubwa kichwani akiwa ndani ya gari.

NSA AKIWA TAABANI KCMC

Taarifa zinaeleza Nsa alipigwa jiwe akiwa ndani ya gari. Waliompiga wanaelezwa kuwa wafuasi wa Chadema ambao walikuwa wamefunga barabara.

Nsa amekuwa mjini Moshi kumuunga mkono Makamu Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Davies Mosha.

Mosha anawania ubunge wa Moshi Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

SALEHJEMBE INAMUOMBEA NSA APATE NAFUU MAPEMA NA KUPONA KABISA.



1 COMMENTS:

  1. Sasa watanzania ndio wajiangalie kama kweli hawa Chadema wana nia njema na nchi yetu,dawa yao ni kutowapigia kura tuu.Wote tuungane kuwakataa hawa wabaguzi wenye shauku la kuleta machafuko hapa nchini.Pole sana Nsa Job mungu atakupigania na in shaa allah utatoka hospital kabla ya siku ya uchaguzi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic