Mshambuliaji wa timu ya Simba, Hamisi Kiiza ndiye mchezaji bora wa Ligi
Kuu ya Vodacom kwa mwezi Septemba.
Kwa kuibuka mchezaji bora, Kiiza atazawadiwa sh. milioni moja kutoka kwa
mdhamini wa ligi hiyo, kampuni ya Vodacom.
Kiiza ambaye ameisadia Simba kufanya vizuri kwenye mwezi huo, ikiwemo
kufunga mabao matatu (hat trick) kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar aliwashinda
washambuliaji wa timu za Stand United (Elias Maguli) na Yanga (Amissi Tambwe).
Ndani ya mwezi Septemba ambapo zilichezwa raundi tano, Kiiza amefunga
jumla ya mabao matano.
0 COMMENTS:
Post a Comment