October 6, 2015


Beki wa Mbeya City, Juma Nyosso amepiga hodi kwenye Chama cha Wachezaji Tanzania (Sputanza) na kuomba kutetewa rasmi.



Nyosso anataka TFF kuangalia upya adhabu yake ya kutocheza kwa miaka miwili pamoja na Sh milioni mbili ikiwa ni baada ya kumshika makalio mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco.

Mwenyekiti wa Sputanza, Mussa Kisoki ambaye mwanzo waliitetea adhabu hiyo, amebadilika na kusema sasa watamtetea Nyosso.

"Hii ndiyo kazi yetu, kweli adhabu tuliiunga mkono lakini hatuwezi kukataa kumtetea mchezaji hasa kama tunaona mambo hayajakaa vizuri," alisema Kisoki.

Kisoki amesema wameona kama kuna tatizo katika hizo katika uamuzi wa jambo hilo na sasa wanataka TFF ipitie upya.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic