October 29, 2015

KERR AKIZUNGUMZA NA WASAIDIZI WAKE, SELEMANI MATOLA NA KOCHA WA MAKIPA, IDDI SALIM KUTOKA KENYA WAKATI WA MECHI DHIDI YA COASTAL UNION, JANA/
Kocha wa Simba, Dylan Kerr amefurahia kikosi chake kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union, jana.


Ushindi huo katika Ligi Kuu Bara umemfanya Kerr aongeze pointi tatu, lakini hajaridhishwa na uchezaji wa kikosi chake.

Kerr raia wa England anaamini Simba ina kikosi bora, lakini hakikuonyesha kandanda safi na ushindi huo ulikuwa sawa na wa kubahatisha.

“Hatukucheza vizuri, hakukuwa na juhudi ya kutosha kuhakikisha ushindi unapatikana.

“Lazima tubadilike na kufanya kazi zaidi. Wanasimba wanategemea mambo mengi yabadilike kupitia kikosi hiki, mimi sinafurahia sana,” alisema.


Simba ilishindwa kuonyesha kiwango bora katika mchezo huo na bahati ilipata bao la mapema kupitia Hamisi Kiiza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic