October 30, 2015


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema Ligi Kuu Bara bado ni ngumu kwao lakini watapambana hadi mwisho.


Yanga inashuka uwanjani kesho kuwavaa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, kesho.

“Ni mechi ngumu sana, kila unayocheza inakuwa ngumu zaidi kwa kuwa timu zinajiandaa kushinda dhidi ya sisi.

“Unajua sisi ni mabingwa, kila timu inaona kutufunga ni sehemu ya kupima ubora walionao. Hivyo naweza kusema tuna kazi mara mbili zaidi ya kila timu,” alisema.

Yanga sasa inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa nyuma ya Azam FC.


Yanga ina pointi 19 alakini Azam FC imefikisha pointi 22 baada ya ushindi wa mabao 4-2 jana dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic