Watanzania
wapenda soka, wengi wanataka kuona kama kweli Tanzania itafanya mapinduzi
Novemba 14 wakiwa wanaivaa Algeria katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la
Dunia.
Mechi
hiyo inapigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na inaonekana washambuliaji
wawili tegemeo, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta wako tayari.
Utayari
unatokana na wenyewe kupiga aina mpya ya unyoaji, wakiwa tayari kuitumikia TP
Mazembe katika Ligi ya Mabingwa Afrika na baada ya hapo wanateremka nchini,
tayari kwa kazi.
Kikubwa
ni kuwaombea uzima wamalize majukumu yao wakiwa na Mazembe salama, ili warejee
kulitumikia taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment