Mshambulizi wa Simba, Mganda, Hamis
Kiiza, amemkaribisha Mrundi wa Azam FC, Didier Kavumbagu, kujiunga na timu hiyo
inayofundishwa na Muingereza, Dylan Kerr.
Hiyo ni siku chache tangu ziwepo tetesi
za Mrundi huyo kuomba kujiunga na Simba kwenye usajili wa dirisha dogo msimu
huu kwa mkopo.
Mrundi huyo, hivi sasa hana nafasi ya
kucheza kwenye kikosi cha kwanza tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu Bara,
kwa kile kinachodaiwa kuwa mshambuliaji huyo ameshindwa kumudu mfumo wa Kocha
Mkuu Muingereza, Stewart Hall.
Kiiza alisema kuwa, anatambua uwezo wa
mshambuliaji huyo ndani ya uwanja, hivyo anaamini akitua kuichezea timu hiyo,
ataiboresha safu yao ya ushambuliaji.
Kiiza alisema kikubwa anataka kuona safu
yao ya ushambuliaji inaimarika kwa kuwepo na washambuliaji wenye uwezo mkubwa
wa kufunga mabao.
“Katika timu lazima wawepo
washambuliaji zaidi ya watatu ambao ni tishio kwa wapinzani, lakini siyo kuwepo
mmoja ambaye mabeki wa timu pinzani wenyewe wanamuangalia yeye tu katika
kumkaba.
“Hivyo kama Kavumbagu anataka kuja
Simba, mimi namkaribisha, ni mshambuliaji mzuri niliyecheza naye timu moja ya
Yanga, ana uwezo mkubwa wa kufunga mabao, pia anajua kupambana,” alisema Kiiza.
0 COMMENTS:
Post a Comment