October 21, 2015

FRIENDS RANGERS
Ligi Daraja la Kwanza iliyoanza kutimua vumbi Septemba 19, mwaka huu, imeonekana kuwa na washambuliaji wenye njaa ya kufunga mabao kutokana na kwamba mpaka sasa mabao 109 yametiwa kimiani.

Mabao hayo yamefungwa huku ligi hiyo ikiwa imeshamaliza raundi ya tano kwa timu zote 24 kushuka dimbani huku ushindani ukionekana kuwa ni wa hali ya juu.

Cha kuvutia zaidi, timu zote nane zilizogawanywa katika makundi matatu, makundi yao kama yanalingana kwani kwenye mabao hayo 109, hayajapishana sana.

Kundi A, linaloongozwa na Ashanti United yenye pointi 10, timu zake nane mpaka sasa zimeshafunga jumla ya mabao 37, huku Kundi B linaloongozwa na Ruvu Shooting yenye pointi 10, lina jumla ya mabao 36, sawa na Kundi C linaloongozwa na Geita Gold Sports yenye pointi tisa.


Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena Oktoba 31, mwaka huu kwa kupigwa mechi 11 huku moja ikitarajiwa kupigwa siku inayofuata kuhitimisha mzunguko wa sita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic