Kocha wa timu ya Taifa ya Oman ya Soka la Ufukweni
(Beach Soccer), Talib Hilal jana ametoa msaada wa mipira 10 kwa ajii ya mchezo
wa soka la ufukweni ambao umeanza kuwa maarufu nchini.
Kesho Jumamos tarehe 10 Oktoba, 2015 kocha Talib
atakutana na makocha, waamuzi wa mchezo wa ufukweni waliopo jijii Dar es salaam
ili kubadilishana uzoefu saa 5 kamili asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa TFF
uliopo Karume.
Kocha huyo amekiwezesha kikosi cha Oman kubeba ubingwa
wa Asia pia kushiriki michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika nchini Ureno
miezi michache iliyopita.
Talib aliwahi kuichezea Simba, pia kuipa ubingwa wa
Ligi Kuu Bara wakati akiwa kocha.
0 COMMENTS:
Post a Comment