October 18, 2015


Beki Juma Nyosso amerejea uwanjani tena siku chache baada ya kufungiwa kucheza soka miaka miwili kutokana na kitendo cha udhalilishaji dhidi ya nahodha wa Azam FC, John Bocco.

Nyosso amerejea uwanjani akiwa nahodha na safari hii akiichezea Team Ismail katika tamasha la Kandanda Day lililofanyika katika Uwanja wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam, jana.

Nyosso aliiongoza timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na tamasha hilo lilifana huku Team Ismail ikilipa kisasi cha kutandikwa katika tamasha la mwaka jana.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic