October 6, 2015



Nahodha wa Chelsea, John Terry amewataka wachezaji wa kikosi hicho kujitoa kwa ajili ya klabu na kocha Jose Mourinho.
Terry amewaambia wachezaji wenzake ni lazima wamuunge mkono kocha Mourinho.


“Hatuwezi kufanikiwa bila ya kumuunga mkono kocha, lazima tupambane kwa ajili ya timu, klabu yetu lakini kocha pia.

“Ni lazima tuhakikishe hatumuangushi, lakini hatuwaangushi mashabiki,” alisema Terry.


Chelsea ambao ni mabingwa wa England wamewakuwa wakienda kwa mwendo wa kusuasua kutokana na kupoteza mechi nne katika nane walizocheza mwanzoni mwa msimu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic