FAROUKH BAGHOZA (KATIKATI) WAKATI ALIPOILETA REAL MADRID YA WAKONGWE |
Katika kuimarisha maandalizi ya Timu ya Taifa (Taifa Stars)
kuelekea katika mashindano mbalimbali ikiwemo mechi mbili za ugenini na
nyumbani dhidi ya Algeria, Rais wa TFF Jamal Malinzi ameunda kamati maalum
itakayoitwa “Kamati ya Taifa Stars” ambayo majukumu yake yatakua:
(i) Kuimarisha huduma kwa wachezaji,
(ii)
Uhamasishaji na Masoko,
(iii)
Kuhamasisha wachezaji,
(iv)
Kuandaa na kusimamia mkakati wa Ushindi.
Kamati
hii itaongozwa na Mwenyekiti Farough Baghouzah, Teddy Mapunda (Katibu), Wajumbe
ni Juma Pinto, Michael Wambura, Iman Madega, Salum Abdallah na Isaac Chanji.
Aidha
Kamati hiyo imepewa jukumu la kuwashirikisha wadau mbalimbali wa mpira wa miguu
katika kutekeleza majukumu hayo.
Wadau
wa mpira wa miguu ambao kamati itashirikiana nao ili wajumuike na kusaidia
majukumu mbalimbali katika kamati hiyo wanaombwa waitikie wito huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment