Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza
viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom siku ya Jumamosi kati ya Yanga SC
dhidi ya Azam utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,
kiingilio vha chini kikiwa ni shilingi elfu tano (5,000) kwa viti vyenye rangi
ya bluu, kijani na Machungwa.
Tiketi za mchezo huo zitauzwa siku ya mchezo Jumamosi
katika eneo la Uwanaj wa Taifa jijini Dar es salaam, ambapo kingilio cha juu
kitakua ni Shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa VIP A, na Shilingi Elfu
Ishirini (20,000) kwa VIP B & C.
Mwamuzi wa mchezo huo atakua Abdallah Kambuzi kutoka
mkoani Shinyanga, akisaidiwa na Makame Mdogo (Shinyanga), Robert Luhemeja
(Mara), mwamuzi wa akiba Frank Komba (Dsm) huku Kamisaa wa mchezo akiwa Joseph
Mapunda kutoka mkoa wa Ruvuma.
Michezo mingine ya Ligi Kuu ya Vodacom siku ya
Jumamosi ni Majimaji FC dhidi ya African Sports katika uwanja wa Majimaji mjini
Songea, Ndanda FC wakiwakaribisha Toto African katika dimba la Nangwanda
Sijaona mjini Mtwara.
Mbeya City FC watawakaribisha Simba SC kwenye dimba la
uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Stand United wakiwakaribisha Tanzania Prisons
kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyaga, Jijini Tanga Coastal Union watakua
wenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Mkwakwani.
Jumapili ligi hiyo itaendelea kwa michezo miwili,
Maafande wa Mgambo Shooting watakua wenyeji wa Kagera Sugar uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga, huku wachimba Almasi wa Mwadui FC wakiwakaribisha JKT Ruvu katika
uwanja wa Mwadui Complex.
0 COMMENTS:
Post a Comment