Azam FC imerejea kileleni baada ya kuitwanga
Toto African kwa mabao 5-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa kwenye Uwanja
wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, leo.
Azam FC sasa imefikisha pointi 25 na kurejea
kileleni juu ya Yanga yenye pointi 23.
Mabao ya Azam FC ambayo ilitawala mchezo leo
yalifungwa na Mrundi Didier Kavumbagu aliyefunga mawili na beki Shomari Kapombe
naye akapachika mawili huku moja likifungwa na Kipre Tchetche.
Wenyeji ndiyo waliotawala mchezo kwa muda
wote kuhakikisha mambo yanakwenda safi kwao na wanarejea kileleni baada ya
kushushwa na Yanga kwa saa kadhaa.
0 COMMENTS:
Post a Comment