Barcelona
sasa haishikiki, kama unabisha waulize AS Roma ya Italia.
Baada
ya kuitwanga Real Madrid mabao 4-0 katika mechi ya La Liga, leo imeangushia
kipigo AS Roma cha mabao 6-1 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mabao
ya Barcelona yamefungwa na Lionel Messi na Luis Suarez ambao kila mmoja
amefunga mawili, Gerard Pique na Adriano kila mmoja akafunga moja.
Eden Dzeko alifunga bao pekee la Roma lakini akakosa kufunga mkwaju wa penalti kama ilivyokuwa kwa Neymar.
0 COMMENTS:
Post a Comment