Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo
‘Julio’ amegonga hodi kwa kikosi cha Azam FC na kumuomba mshambuliaji wa timu
hiyo Kelvin Friday ambaye amekuwa hana nafasi ndani ya kikosi hicho kwa sasa.
Mpaka sasa Mwadui bado
haijafanikiwa kumsajili mchezaji yeyote ingawa ina mpango wa kusajili wachezaji
kadhaa kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye timu hiyo.
Julio alisema anahitaji kuboresha kikosi
chake ndiyo maana ameamua kumchagua mshambuliaji huyo wa Azam.
Julia alisema anahitaji kuwa na kikosi
chenye ushindani na kuhakikisha safu yake ya ushambuliaji inakuwa imara.
“Ni kweli namhitaji Kelvin Friday yule
wa Azam wakinipatia yule atanifaa sana ndani ya kikosi changu kwa sababu
ninahitaji kukiboresha kidogo hasa kwenye safu ya ushambuliaji,” alisema Julio.
0 COMMENTS:
Post a Comment