November 12, 2015


Kocha mkongwe, Carlo Ancelotti anayepewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi ya Jose Mourinho amefunguka kwa mara ya kwanza na kusema, wachezaji Chelsea ndiyo tatizo.


Ancelotti amekiri anegpenda kufanya kazi England, lakini akasisitiza, Mourinho hana kosa kama wachezaji watashindwa kujihamasisha wao binafasi.

“Kweli wachezaji wanapaswa kuhamasishwa, hii ni kazi ya kocha. Lakini Mourinho hawezi kufanikiwa kama wachezaji watashindwa kujihamasisha wao wenyewe.

“Naona kama msimu uliopita Chelsea walichukua ubingwa kiulauni sana. Huenda msimu huu suala la uhamasishaji halikupewa nafasi. Lakini katika hili la kufanya vibaya, wachezaji hawawezi kujiweka kando,” Ancelotti aliliambia Sportsmail la Uingereza.


“Pamoja na yote, katika soka wakati mwingine yanatokea mambo, hauwezi hata ukaelezea. Kumbuka Istambul nikiwa AC Milan, hadi mapumziko tulikuwa mbele kwa mabao 3-0. Lakini kipindi cha pili tukaruhusu mabao matatu, ikawa sare na mwisho Liverpool wakachukua kombe.”


MAKOMBE LUNDO ALIYOBEBA ANCELOTT

Juventus (1999-2001)
·       Intertoto Cup 1999 

AC Milan (2001-2009)
·       Champions League 2002-03, 2006-07 
·       UEFA Super Cup 2003, 2007
·       Coppa Italia 2002-03 
·       Serie A 2003-04
·       Supercoppa Italiana 2004
·       Club World Cup 2007 

Chelsea (2009-2011)
·       Community Shield 2009
·       Premier League 2009-10
·       FA Cup 2009-10 

Paris Saint-Germain (2011-2013)
·        Ligue 1 2012-13

Real Madrid (2013-2015)
·       Copa del Rey 2013-14 
·       Champions League 2013-14
·       UEFA Super Cup 2014

·       Club World Cup 2014 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic