November 12, 2015


Rais John Pombe Magufuli ameipa soka heshima kubwa kabisa na itakuwa ni ya aina yake tokea aliposhinda kiti hicho, mwezi uliopita.


Magufuli amekubali kuwa mgeni rasmi katika mechi ambayo Taifa Stars inakutana na wababe wa Afrika, Algeria keshokutwa Jumamosi.

inakuwa ni rekodi kwa kuwa Rais Magufuli hakuwa amekwenda kwenye hafla yoyote kubwa ukiachana na zile zake za kushtukiza katika Wizara ya Fedha na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Lakini wapenda soka watajumuika na Magufuli kwa mara ya kwanza tena akiwa ni rais aliyehudhuria mechi ya soka siku chache zaidi baada ya kuchaguliwa kwake.

Mara nyingi, marais waliopita, suala la michezo au soka lilifuatia baadaye sana.

Lakini Magufuli ambaye alikuwa anaelezwa kwamba si mpenda michezo, mapema kabisa amejumuyika na Watanzania wapenda soka kwa kuwa mgeni rasmi.

Taifa Stars iliyokuwa imeweka kambi nchini Afrika Kusini imerejea jana usiku na kwenda moja kwa moja kambini.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic